Simba inatarajia kurejea mazoezini kujiandaa na mechi yake ya Ligi Kuu Bara inayofuatia ambayo itakuwa ni dhidi ya Mbeya City.
Pamoja na kuanza mazoezi kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam, Simba itatoa zawadi ya mchezaji bora wa mwezi.

Kawaida Simba imekuwa ikitoa zawadi kwa mchezaji bora kila mwezi ambaye anapatikana kupitia kura zinazopigwa na mashabiki wake kupitia mtandao.


Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema mchezaji bora wa mwezi atalamba Sh 500,000.

"Mchezaji bora wa mwezi uliopita anatangazwa leo pale kwenye mazoezi yatakayofanyika kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam," alisema Manara.

Advertisement

 
Top