Kamati ya Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania zinazotolewa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) imepitia majina ya wanamichezo waliopendekezwa kuwania tuzo hizo mwaka huu huku Nahodha wa Yanga na Taifa Stars Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akipambanishwa na beki Erasto Nyoni wa Azam FC na mshambuliaji Elia Maguli wa Simba. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati hiyo, Rehure Nyaulawa, kamati ilikutana jijini Dar es Salaam jana na tuzo zitatolewa Desemba 12, mwaka huu jijini zikihusisha wanamichezo waliofanya vizuri kati ya Juni 2013 hadi Juni 2014. Amesema zaidi ya wanamichezo 40 watakabidhiwa tuzo zao siku hiyo na kamati imejiridhisha kuwa wanaowania tuzo hizo wanastahili kulingana na mapendekezo ya vyama vya michezo kupitia kamati zake za fundi. Mshindi wa kila tuzo ataingia katika mchakato wa kumpata Mwanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 2013/2014. Kutatolewa pia zawadi ya Tuzo ya Heshima kwa yule ambaye itaonekana alikuwa na mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya kimichezo nchini.
                                                                                   
ORODHA KAMILI WANAOWANIA TUZO ZA TASWA 2013/14
OLIMPIKI MAALUM: Wanaume:
Raphael Kalukula, Pazi Mwinyimkuu na Hatibu Matali wanawake: Blandina Blasi, Shida Jaha na Mwanaharusi Risasi
MPIRA WA KIKAPU: Wanaume:
Lusajo Samwel (Oilers), Erick Mchemba (ABC) Wanawake: Sajda Ahmed Lyamaiga(Don Bosco Lioness), Rehema Silomba (Don Bosco Lioness) na Orlyn Titus (Don Bosco Lioness)
MPIRA WA MAGONGO: Wanaume:
Yohana Wilson, Focus Paul, Deep Vaja Wanawake: Valentina Quarantta, Kidawa Seremala na Mary Mhina
MPIRA WA WAVU: Wanawake:
Yasinta Remmy (Jeshi Stars), Hellena Richard (Magereza) na Teddy Abwao (Jeshi Stars) WanaumE: Kelvin Peter Severino (Magereza), Nassoro Sharifu (Jeshi Stars) na Athuman Rupia (Jeshi Stars)
RIADHA: Wanawake:
Zakia Mrisho, Jaqueline Sakilu na Catherine Lange Wanaume: Alphonce Felix, Dickson Marwa na Fabian Nelson
BAISKELI: Wanawake:
Salome Donald, Martha Anthon na Sophia Adson Wanaume: Richard Laizer, Hamisi Mskala na Gerald Konda.
GOFU: Wanaume:
Nuru Mollel, Abasi Adam na Frank Mwinuka Wanawake: Madina Iddi, Hawa Wanyeche na Angel Eaton
GOFU YA KULIPWA:
Hassan Kadio, Yassin Salehe na Geoffrey Leverian
JUDO Wanaume:
KOMBO Masoud Amour, MBAROUK MbaroukSleiman Wanawake: Grace Alfonce Mhanga, Salma Omari Othman
TENISI WALEMAVU Wanaume:
Novatus Emmanuel Temba, Yohana Assa Mwila, Juma Mohamed Hamisi Wanawake: Rehema Selemani Saidi,Bihawa Mustafa Ituji
TENISI Wanaume:
Tumaini Martin, Emmanuel Malya na Omari Sulle Wanawake: Rehema Athumani, Edna John, Georgina Kaindoh
NETIBOLI
Doritha Mbunda (JKT Mbweni), Berina Kazinja (Magereza Moro), Andressa Andrea (Magereza Moro)
Ngumi za Ridhaa:
Fabian Gaudence, Ahmed Furahisha na Ally Abdul Ahmed
SOKA Wanawake
Sophia Mwasikili, Sherida Boniface na Amina Ally
WANAUME Elias Maguli (Ruvu Shooting-sasa Simba), Erasto Nyoni (Azam FC) na Nadir Haroub (Yanga).
WACHEZAJI WA NJE WANAOCHEZA TANZANIA
Kipre Tchetche (Azam), Amis Tambwe (Simba) na Mbuyu Twite (Yanga).
WATANZANIA WANAOCHEZA NJE
Richard Laizer (baiskeli-Afrika Kusini/Uswisi) Mbwana Sammata (TP Mazembe-soka DRC), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe-soka DRC).
NGUMI KULIPWA,
Francis Cheka, Ramadhani Shauri na Said Mbelwa.
MPIRA WA MIKONO
Wanaume: Hemedi Salehe (JKT), Msafiri Makoti (Ngome) na Abinery Kusena (JKT) Wanawake: Veronica Mapunda, Subira Omary na Mwajabu Lugato
WANAMICHEZO CHIPUKIZI
Omari Sulle (tenisi) Sheridah Boniface (soka wanawake) Aishi Manula (soka wanaume- Azam FC)

Advertisement

 
Top